Misa Elizabeti Lyrics

MISA ELIZABETI

UTUHURUMIE

 • Bwana Bwana, Bwana tuhurumie *2
 • Kristu Kristu, Kristu tuhurumie *2
 • Bwana Bwana, Bwana tuhurumie *2

UTUKUFU (MT. ELIZABETI)

Utukufu kwa Mungu juu, na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi mema *2

 1. Tunakusifu tunakuheshimu -
  Sifa ni kwako milele yote
  Twakuabudu, tunakutukuza -
  Twakushukuru kwa utukufu -
  Mfalme wa mbingu, Baba Mwenyezi -
 2. Yesu Kristu, mwana wa pekee -
  Mwanakondoo, mwana wake Baba -
  Uondoaye dhambi za dunia -
  Utuhurumie utusikilize -
 3. Unayeketi kuume kwa Baba -
  Mtakatifu mkuu Yesu Kristu -
  Na pamoja naye Roho Mtakatifu -
  Ndaniye Baba. Amina. Amina.

  NINASADIKI (MT. ELIZABETI)

  Ninasadiki kweli ninasadiki (kweli) ninasadiki *2

  1. Mungu Baba mwumba vyote, ninasadiki
   Na mwanawe Yesu Kristu, ninasadiki
   Mkombozi wa watu wote, ninasadiki
   Ni mzaliwa na Maria, ninasadiki
  2. Alikufa msalabani. . .
   Kwa ajili yetu sisi . . .
   Siku ya tatu kafufuka . . .
   Alipaa mbinguni . . .
  3. Yuko kuume kwa Baba . . .
   Atakuja kuhukumu . . .
   Naye Roho Mtakatifu . . .
   Ndiye mleta wa uzima . . .
  4. Na Kanisa Katoliki . . .
   Takatifu la mitume . . .
   Naungama ubatizo . . .
   Ufufuko na uzima . . .

   BABA YETU ( MT. ELIZABETI)

   Baba yetu wa mbinguni (jina)
   Jina lako litukuzwe daima

   1. Ufalme wako utufikie,
    Duniani kama mbinguni (Baba)
   2. Utupe leo riziki zetu,
    Utusamehe makosa yetu (Baba)
   3. Kama tunavyowasamehe,
    Wale waliotukosea (Baba)
   4. Usitutie kishawishini,
    Utuopoe maovuni (Baba)
   5. Kwa kuwa ufalme ni wako Baba,
    Na nguvu na utukufu (Baba)
   Misa Elizabeti
   CATEGORYMisa (Sung Mass)
   • Comments