Misa Migori Lyrics

MISA MIGORI

@ Afred Ossonga

  BWANA TUHURUMIE

 1. Bwana tuhurumie, tuhurumie ewe Bwana Aah aah ah Bwana
  Tuhurumie ewe Bwana
 2. Yesu Kristu tuhurumie . . .
 3. Bwana tuhurumie

  UTUKUFU KWA MUNGU (MIGORI)

  Utukufu kwa Mungu juu na amani duniani
  Na amani kwa watu wote (wenye)
  { Wenye mapenzi mema, watu wenye mapenzi mema
  Wenye mapenzi Watu (wenye) mapenzi mema }*2

 1. Tunakusifu tunakuheshimu
  Tunakuabudu tunakutukuza
  Tunakushukuru kwa ajili ya
  Utukufu wako, wako mkuu
 2. Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni,
  Mungu Baba mwenyezi ee Bwana Yesu Kristu,
  Mwana wa pekee, ee mwana Mungu
  Mwanakondoo wa Mungu, mwana wa Baba
 3. Mwenye kuondoa dhambi za dunia
  Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
  Pokea ombi letu ewe mwenye kuketi
  Kuume kwa Baba, utuhurumie
 4. Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako
  Peke yako mkuu ee Bwana Yesu Kristu
  Pamoja na Roho Mtakatifu
  Katika utukufu, wa Mungu Baba amina
Misa Migori
COMPOSERAfred Ossonga
CATEGORYMisa (Sung Mass)
 • Comments