Wakristu Wote Simameni Lyrics

WAKRISTU WOTE SIMAMENI

@ Ochieng Odongo

 1. Wakristu wote simameni, simameni
  Tuchezeni mbele za Bwana, kwa shukrani

  (Leo) Asubuhi na mchana nitamsifu (Bwana)
  Na usiku nitaita jina la Bwana (wangu)
  Sifa zake zi kinywani mwangu daima
  Nitaimba sifa zake Mungu milele

 2. Tupeperusheni mikono juu hewani
  Tushangilieni tupigeni makofi
 3. Ametulisha kwa chakula cha mbinguni
  Twaburudika kwa kinywaji cha uzima
 4. Ametukinga na maovu ya dunia
  Mapenzi yake kwetu sisi ni ya ajabu
 5. Turukeruke na tucheze kama ndama
  Tupigeni ngoma kayamba na vinanda
Wakristu Wote Simameni
COMPOSEROchieng Odongo
CHOIRSt. Benedict Rapogi
ALBUMMbegu Nyingine (Vol 2)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments