Sadaka Yetu Bwana

Sadaka Yetu Bwana
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerDan Odhiambo
Views4,725

Sadaka Yetu Bwana Lyrics

  1. Sadaka yetu Bwana, twaomba upokee
    Ni mazao ya mashamba yetu ee Baba upokee *2

  2. Mkate na divai, na pia nafsi zetu
    Ni zawadi yetu kwako, ee Baba upokee
  3. Na fedha za mifukoni,mazao ya mashamba,
    Ee Baba, kazi zetu, twaomba upokee(sadaka)
  4. Pokea na nyoyo zetu, miili yetu pia
    Ee Baba utupokee, tulio wana wako(sadaka)
  5. Pokea tunakuomba, ingawa ni kidogo
    Kwa unyenyekevu Baba, tunavileta kwako
  6. Zawadi hii twaitoa, kwa sifa yako wewe,
    Kwa ajili yetu sisi, nazo jamaa wetu (sadaka)