Login | Register

Sauti za Kuimba

Nitakushukuru kwa Moyo Wangu Wote Lyrics

NITAKUSHUKURU KWA MOYO WANGU WOTE

@ Elias Majaliwa

{ Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote } *2

{ Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi
Nitashukuru nikilikabili hekalu lako
Hekalu lako hekalu lako takatifu
Nitalishukuru jina lako Bwana (Bwana) *2 } *2

 1. Kwa ajili ya fadhili na uaminifu wako
  Wewe Bwana umeikuza ahadi yako
  Kuliko jina lako na nilipokuita
  Uliitika ukanifariji nafsi
 2. Ee Bwana wafalme wote watakushukuru
  Watakaposikia maneno ya kinywa chako
  Naam wataziimba njia zako Bwana
  Kwa maana utukufu wako ni mkuu
Nitakushukuru kwa Moyo Wangu Wote
COMPOSERElias Majaliwa
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMHaya Tazameni (Vol 21)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments