Nitakusifu Mungu

Nitakusifu Mungu
ChoirSt. Don Bosco Kyaani
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerFrt. Tailo M

Nitakusifu Mungu Lyrics

 1. { Nitakusifu Mungu(Mungu) Mwenyezi
  Kwa mema mengi Baba unayoyatenda } *4
  { Unastahili sifa milele (Bwana)
  Utukufu na sifa zako milele } *2

 2. Furaha yangu ni kubwa ee Mungu kukusifu kwa nyimbo nzuri na sala
  Unipe neema zako ee Mungu niongoze katika maisha yangu
 3. Mbingu zahubiri utukufu Mungu wangu bila uoga wowote
  Anga yaitangaza kazi ya mikono yako ee Mwenyezi uliye juu
 4. Fadhili zako ni za milele na uaminifu wako haupimiki
  Nitaimba zaburi yako Bwana siku zote za maisha yangu