Mtazame Mkombozi Msalabani

Mtazame Mkombozi Msalabani
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)

Mtazame Mkombozi Msalabani Lyrics

Mtazame Mkombozi msalabani,
Tazama mikono na miguu, vimefungwa kwa misumari
Mtazame Mkombozi msalabani,
Tazama ubavu wake, ulivyochomwa kwa mkuki

 1. Msilie enyi kila mama, msinililieni mimi
  Bali watoto wenu, pia nafsi zenu
 2. Mateso gani haya ee Bwana, unayoteseka Mungu wangu
  Lipi baya ee Bwana ulilolitenda
 3. Hatia hiyo wanaiunda, hukumuni wanakuingiza
  Nawe hujibu neno, wakubali kufa
 4. Nguvu mwilini zimekutoka, mara ya tatu unaanguka
  Teso kubwa ee Bwana, lakusonga sana
 5. Juu msalabani unalia, mateso yamezidi sana
  Wasema nina kiu, wanakupa siki