Yesu Kashinda Kifo

Yesu Kashinda Kifo
ChoirSt. Monica Sinza
AlbumNi Siku Njema Leo
CategoryPasaka (Easter)
Composer(traditional)

Yesu Kashinda Kifo Lyrics

 1. Yesu kashinda kifo, kafufuka leo mfalme wa watu wote
  Yesu kashinda kifo, njooni tumwimbie kwa shangwe
  Sisi wadhambi alitupenda, katuokoa kaleta na amani
  Tuufurahie wema wake njooni wote tukamsifu
 2. Tufurahi pamoja, Yesu ameshinda nguvu zake shetani
  Tufurahie leo, kweli katuokoa sote
  Yeye ni Mungu pia Mwokozi, msalabani katuokoa sote
  Tuikumbuke huruma yake, tuikumbuke siku zote
 3. Umeshinda mauti, Yesu umetoka kaburini mzima
  Umeshinda mauti, ewe Yesu nakuamini
  Ewe Mungu wangu siku zote, unanipenda ingawa nina dhambi
  Unijalie neema yako nikufuate siku zote