Sadaka Yangu

Sadaka Yangu
ChoirTBA
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerFr. A. Kauki

Sadaka Yangu Lyrics

Sadaka yangu, kwako ee Mungu
Ni moyo mnyofu na uliopondeka
Tazama wapendezwa na kweli ya moyo
Nawe wanijulisha hekima kwa siri
Nioshe kabisa na uovu wangu wote
Na kinywa changu kitanena sifa zako

 1. Maana wewe Bwana hupendezwi
  Na dha-bihu za kuteketezwa
  Ama- sivyo mimi ningalikutolea
 2. Wapendezwa na dhabihu za haki
  Kuto-ka- kwa moyo mnyofu
  Zitolewazo juu ya madhabahu yako
 3. Ee Mungu wa wokovu wangu
  Unipe moyo radhi wa utii
  Usiniondolee Roho wako Mtakatifu

Favorite Catholic Skiza Tunes

Composer: Fr. Kauki