Twende kwa Yesu Lyrics

TWENDE KWA YESU

@ John Sway

 • Nakualika nakualika nawe ndugu yangu
  Njoo twende kwake Bwana Yesu (twendeni)
  Tukamueleze shida zetu zote (Yeye) anaweza yote
  { Matatizo yetu - tukampe Yeye, tukampe Yeye atatufariji } *2

---MASHAIRI---

 1. Yeye mwenyewe alisema,
  Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao
  Na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha
 2. Yeye mwenyewe alisema,
  Ombeni ombeni ombeni mtapewa
  Tafuteni mtapata, bisheni hodi mtafunguliwa
 3. Tujikabidhi mbele zake,
  Bwana Yesu atatuponya na magonjwa
  Magonjwa ya mwili na roho, tukiwa na imani kwake

---HITIMISHO---

 • Unangoja nini wewe twende (twende) twende (twende) kwa Yesu
  Wala usiogope wala usisitesite,
  { Twende pamoja, usibaki nyuma, twende } *2
Twende kwa Yesu
ALT TITLENakualika Nakualika
COMPOSERJohn Sway
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
MUSIC KEYE
TIME SIGNATURE6/16
SOURCEBMTL K/Ndege Dodoma
 • Comments