Yesu ni Mwangaza

Yesu ni Mwangaza
Alt TitleMwangaza
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerBernard Mukasa
VideoWatch on YouTube
Views5,202

Yesu ni Mwangaza Lyrics

  1. Ndipo ukatema mate, aridhini, ukalifanya tope, mkononi
    Ukampaka kipofu , ma-choni, macho yakafunguka, akaona,
    Na mimi ni kipofu, nifumbue, macho ya roho yangu, kwa maana

    {
    { / s/ Mwangaza ni wewe, Mwokozi ni wewe
    Mwalimu ni wewe, Kiongozi ni wewe
    / w / Ni wewe mwangaza na ni wewe Mwokozi
    Ni wewe mwalimu na ni wewe kiongozi
    } *2 Yesu
    } *2

  2. Ukamshusha kutoka, kwenye mti, Yule mtu mfupi, wa ushuru
    Ukala nyumbani mwake, Zakayo, na ukamfundisha, kugeuka
    Naye akakusikia, mwalimu, kageuza mwenendo, kwa maana
  3. Naomba niongoze, ee Yesu, nibadili mwenendo, nigeuke
    Njia inipotoshayo, niiache, uniponye usugu, wa moyoni
    Dhambi niirudiayo, niishinde, nifundishe niweze, kwa maana