Natazama Kalvari

Natazama Kalvari
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerGabriel Kapungu
SourceMbeya
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyA

Natazama Kalvari Lyrics

 1. Nimekukosa Bwana, kwa moyo wote ninajuta kweli, kwa moyo wote
  Roho yangu ina-yohuzunika ninapokuona ulivyokufa

  { Natazama Kalvari (Bwana) ulivyotundikwa mtini (kweli)
  Mwili wangu wanyong'onyea ulivyosulibiwa } *2

 2. Tena ni mimi Bwana, ni dhambi zangu ulizozifia, msalabani
  Kifo cha aibu, kilikufika makusudi mimi, niokolewe
 3. Kwenye kilima kile, walikusonya wakisema wote, asulibiwe
  Kifo chako kwetu ni ukombozi wa mioyo yetu, na roho zetu
 4. Unitulize Bwana, kwa mkono wako kwani ninatubu, makosa yangu
  Naanguka kwako kifudifudi, ninaomba toba, kwa moyo wote