Login | Register

Sauti za Kuimba

Nani Utamtumikia Lyrics

NANI UTAMTUMIKIA

@ Gabriel Nghonoli

{
Chagueni hivi leo mtakayemtumikia
Chagua utakayemtumikia ni nani
Lakini mimi na nyumba yangu, (lakini) mimi (na nyumba yangu)
lakini mimi na nyumba yangu, nitamtumikia Bwana } *2

 1. Pengine mwenzangu, waitumikia miungu
  Unapopata shida, wakimbilia tunguri,
  Waisahau ahadi yako ya ubatizo
 2. Pengine mwenzangu, waitumikia tamaa
  Maisha yako yote yametekwa na mali
  Waithamini mali badala ya Mungu wako
 3. Mtumikie Mungu, mtegemee siku zote
  Achana na miungu, waganga wa kienyeji
  Kwani Mungu pekee ndiye muweza wa yote
Nani Utamtumikia
COMPOSERGabriel Nghonoli
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYE
TIME SIGNATURE6
16
SOURCEKigoma
 • Comments