Login | Register

Sauti za Kuimba

Maneno Tu Lyrics

MANENO TU

@ Charles Ruta

Hohohohoho maneno hohohohoho maneno tu *2
Hoo hoo maneno ohoo bila matendo x2
Nampenda Mungu ( maneno tu )
Nampenda Mungu (maneno tu) hayooooo

 1. Kutwa kucha maneno tu familia yako inayumba amani imetoweka hiyo..
  Umeitelekeza unaponda mali kwa anasa huna wasiwasi,
  Umeiangamiza unaponda mali weee- eti nampenda Mungu eeh, ehee, maneno tu
 2. Kutwa kucha maneno tu hupatani na jirani yako hata salamu hampeani,
  Matatizo yake wayashabikia kwa furaha huna wasiwasi,
  Nazo shida zake wazishangilia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu
 3. Kutwa kucha maneno tu madaraka yako ni ya uma, unayafuja unavyopenda,
  Hauwajali watu wanaoteseka waliao huna wasiwasi
  Hauwajali watu wanaoumia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu

  ~ ~ ~

  Tena nampenda Mungu wangu- nampenda nampenda kuliko kitu chochote
  Na jirani yangu nampenda- nampenda kama nafsi yangu.
  Ni amri ya Mungu( tena) ndiyo amri kuu,
  lakini matendo yako hayafanani na maneno,
  unang'ara uso wako, moyoni unang'ata meno,
  Tazama, matendo, matendo yako, tazama mwenendo, mwenendo wako( aiyooo)
  Ndugu acha maneno,( ooh hayoo) maneno tu,
  Upendo ni matendo (na kabisa ni) matendo
  Ndugu acha maneno (ooh acha) maneno tu,
  Upendo ni matendo ( na kabisa ni ) matendo *2
Maneno Tu
COMPOSERCharles Ruta
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMimina Neema
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYE
TIME SIGNATURE2
4
 • Comments