Kwa Nini Nisiende Lyrics

KWA NINI NISIENDE

 1. Na nyumbani mwake Bwana, nani ataingia
  Bwana yuko mlangoni, atungoja tuingie
  Twendeni wote kwake, tumtolee ibada kweli

  Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
  Niingie nyumbani mwake
  Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
  Nishiriki karamuye
  Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
  Nimshukuru Muumba wangu

 2. Kina baba tuingie, kina mama tuingie
  Tukamuimbie Bwana, nyimbo nzuri za furaha
 3. Vijana tuingie, na watoto tuingine
  Tukamuimbe Bwana, nyimbo nzuri za furaha
 4. Makasisi tuingie, na watawa tuingie
  Tukamuimbe Bwana, nyimbo nzuri za furaha
 5. Tupige vigele gele, kayamba ngoma tucheze
  Kuruka pia turuke, shingo na zinesenese
Kwa Nini Nisiende
CHOIRSt. Bakhita Eastleigh
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments