Login | Register

Sauti za Kuimba

Fumbueni Vinywa Lyrics

FUMBUENI VINYWA

@ D. Wasonga

{ Fumbueni vinywa vyenu (fumbueni) mkapaze sauti zenu
mkisifu mkishangilia ukuu wa Bwana Mungu wetu
Mkirukaruka huku mkiimba sifa za Bwana Mungu wetu } *2
{ Pazeni sauti (pazeni sauti) mkiimba kwa furaha
Fanyeni shangwe kwa zaburi ngoma hata na matari } *2

 1. Tukuzeni sifa zake, tukuzeni sifa zake,
  imbeni imbeni zaburi imbeni zaburi
  Pigeni kelele za shangwe kwa furaha
  Msifuni Mungu wenu kwa kinanda na kinubi
 2. Kwa maana kusifu kwapendeza, kusifu kwapendeza
  Basi njooni tumsifu Bwana Mungu wetu
Fumbueni Vinywa
COMPOSERD. Wasonga
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYA
TIME SIGNATURE2
4
 • Comments