Login | Register

Sauti za Kuimba

Hazina ya Mbinguni Lyrics

HAZINA YA MBINGUNI

@ D. Wasonga

Hiki ndicho nilichoandaa, siku ya leo
(Nami) nakusihi ukipokee
Hii ndiyo shukrani yangu, sehemu ya pato langu
Itokayo ndani ya mtima wangu

Hivyo, naileta mikononi mwako (ambapo) nondo hawataiharibu (na kutu)
Naileta mikononi mwako, ambapo mwizi hawezi kuiba
naileta mahali salama iwe hazina yangu mbinguni

  1. Ninakutolea moyo wangu wala si mifuko yangu
    Ndiyo kazi ya mikono yangu, nakusihi uibariki
  2. Hata kama ni kidogo nakusihi ukipokee
    Kwani ndicho nilichoandaa kukutolea ee Mungu wangu
  3. Hiki ninachokutolea kikekupendeze Mungu wangu
    Kama ile sadaka ya mtumishi wako, mtumishi wako Abeli
Hazina ya Mbinguni
COMPOSERD. Wasonga
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYD
TIME SIGNATURE2
4
  • Comments