Asante Yesu

Asante Yesu
Choir-
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerZacharia Gerald

Asante Yesu Lyrics

1. Ingawa ni Mungu na tena ni mfalme, umejinyenyekeza kwa wadogo sisi
Ulishuka kwetu kukaa na sisi, unabaki kwetu daima katika Ekaristi

Asante Yesu (aleluya) kwa wema wako (aleluya)
Asante Yesu (aleluya) asante sana (aleluya)
Kujitoa kwetu (aleluya) ukawa chakula, asante Yesu, asante sana
Kujifanya kwetu (aleluya) kinywaji cha roho, asante Yesu, asante sana

2. Tulapo mkate huu wa uzima, tunapata uzima tena wa milele
Tunywapo kikombe hiki cha wokovu, twatangaza ufufuko wako uliye tukomboa

Kila nikikutafakari, nikiwaza upendo wako kwangu nasema
Asante Yesu asante,
Yote unayonitendea, asilani siwezi elezea,
Ee Yesu asante, Yesu asante
Unatufundisha upendo, tuwajali wote wakubwa pia wadogo
Asante Yesu asante
Leo hii umetukuka, ninaomba nami unijaze baraka
Asante Yesu Asante

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442