Acheni Kukata Tamaa
| Acheni Kukata Tamaa | |
|---|---|
| Performed by | St. Cecilia Mirerani |
| Album | Maajabu ya Mungu |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Bernard Mukasa |
| Views | 23,083 |
Acheni Kukata Tamaa Lyrics
{Mwenyezi ameniumba, akanileta kati yenu,
Niwakumbushe watu wake thamani yenu duniani} *2
{Acheni acheni kufa moyo,
Acheni acheni kukata tama
Yeye aliyewaumba anaijua kazi yake } *2- Aliijua siri yenu hata kabla hamjaumbwa,
Ramani ya maisha yenu, yote imo mikononi mwake
Magonjwa yanayowatesa na maumivu yasiyokoma,
Ni madogo kuliko yale aliyoyaponya kwa sekunde - Hali mbaya ya kiuchumi, mlo mmoja madeni mengi
Ni njia ya kunyenyekea na kumpa Mungu ukuu
Misiba inayowaliza mnapofiwa na ndugu zenu,
Ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi - Maumivu ya kuonewa kudhulumiwa kusingiziwa
Ni nafasi ya kusamehe na kujivika utakatifu
Matatizo ya ndoa zenu na migogoro ya familia,
Ni bahati mmejaliwa ya kujifunza uvumilivu - Bebeni misalaba yenu, nyamazeni msinung'unike
Huo ndio wokovu wenu shikilieni msiachie