Acheni Mimi

Acheni Mimi
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMshike Mshike (Vol 5)
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerJ. C. Shomaly
Views8,476

Acheni Mimi Lyrics

 1. { Acheni mimi, nimuimbie Muumba wangu,
  Aliyeniumba, mimi kiumbe mwenye akili } *2
  Aliyenipa uwezo wa kusimama hapa
  Tangu tumboni mwa mama amenipa uhai
  Juzi jana leo nimeamka kesho ajua yeye
  Maisha yangu ayapa maziwa ni kama mtoto
  { Acheni mimi, nizitamke sifa za Mungu wangu
  Na sitachoka, kumuimbia mimi ningali hai } *2

 2. [ b ] Nalala jioni na kuamka pia nazo nguvu,
  Ninafanya kazi na kujipatia riziki zangu
 3. Amenipatia akili yangu na wangu ubunifu,
  Shuleni kazini ninayoyafanya hayana pungufu,
 4. Mara nyingi sana ninajiuliza nitampa nini,
  Kwani Bwana amenitendea mengi bila ya kwa nini
 5. Ninapokuwa nazo shida nyingi hunipa tulizo,
  Kwake kila mara watu wote hupata burudiko.