Alhamisi Kuu
Alhamisi Kuu | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Alhamisi Kuu |
Composer | (traditional) |
Views | 12,148 |
Alhamisi Kuu Lyrics
- Alhamisi kuu Yesu alituwekea
Ekaristia takatifu, chakula cha rohoTuimbe - tuimbe,
Tumshukuru - tumshukuru Yesu, mkombozi wetu
Tuimbe - tuimbe,
Tumshukuru - tumshukuru Yesu, sadaka yetu - Yesu alishika mkate akaubariki
Akawapa wafuasi, ndio mwili wangu - Na kikombe cha divai akakibariki
Akasema, nyweni nyote, ndiyo damu yangu - Yesu aliwapa amri wanafunzi wake
Fanyeni hivi daima kwa kunikumbuka - Kisha Yesu akaenda apate kuteswa
Akafuta dhambi zetu msalabani juu - Yesu anatutolea mwili na damuye
Naye Baba wa mbinguni anatubariki
Wimbo huu unaweza kuimbwa Siku ya Alhamisi Kuu au wakati wa Komunyo