Amelaaniwa Mtu Yule
Amelaaniwa Mtu Yule Lyrics
Bwana asema hivi
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu
Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
(Na moyoni mwake amemwacha Bwana
Na moyoni mwa-ke amemwacha Bwana *2)
- Kwa maana yeye atakuwa kama vile fukara nyikani
Naye ataona siku zote yote mema yatendwayo
- Yeye ataishi maisha ya jangwani na yaliyo na ukame
Kwenye nchi kavu, yenye chumvi isiyokuwa na watu
- Kama vile kware asanyaye makinda asiyoyazaa
Ni sawa na yule apataye mali wala si kwa haki
- Amebarikiwa mtu yule amwitaye Bwana ndiye njia,
Ndiye tumaini lake yeye siku za maisha yake