Amezaliwa Masiya wetu
   
    
     
         
          
            Amezaliwa Masiya wetu Lyrics
 
             
            
- Amezaliwa Masiha wetu, hoyee hoye hoye
 Mwana wa Mungu mkombozi wetu, hoyee hoye hoye
 Leo kazaliwa naye Maria na amelazwa
 kwenye hori la wanyama, twende tukamwone
 Amekuja kwetu mwana wa Mungu kuzichukua
 dhambi zetu wanadamu, mkombozi wetu
 { Tumsujudie Bwana Mungu, kwa vigelegele
 Tucheze ngoma na kayamba tupige makofi } *2
- Amelala manyasini, twendeni tukamwone,
 Tukamsalimie Mkombozi wetu
 Kwa zawadi zetu za dhahabu uvumba na manemane
- Wachungaji waondoka, waenda Bethlehemu,
 Wakamsujudie Bwana Mkombozi,
 Wafurahi naye pamoja na Maria naye Yusufu
- Malaika wamefika wengi na wa mbinguni
 Tukajiunge nao tuimbe pamoja utukufu uwe
 Kwa Mungu juu amani kwa watu wenye mapenzi mema
- Tumpokee mkombozi Masiha amekuja
 Ewe mtoto Yesu ishi ndani yetu, tuangaze sisi,
 Kwa mwanga wako mwanga wa Mbinguni.