Amkeni Tufanye Shangwe

Amkeni Tufanye Shangwe
ChoirSt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerAlfred Ossonga

Amkeni Tufanye Shangwe Lyrics

Amkeni wapenzi tufanye shangwe
(Kweli) hekaluni mwa Mungu wetu
Amkeni wapenzi tufanye shangwe
(Kweli) hekaluni mwa Mungu wetu
{Kwa vigelegele, na kwa makofi,
Kwa machezo pia kwa nderemo
Tumsifu Yahweh Jehova leo asubuhi *2}

 1. Waumini wote wenye moyo safi njooni tuingie kwa Bwana
  Njooni tuabudu njooni tusujudu pia tupigeni makofi
  Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo
  Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie
 2. Enyi Baba njooni tusali pamoja ndani ya nyumba yake Baba
  Enyi mama njoni pigeni kelele mbele za Bwana Mungu wetu
  Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo
  Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie
 3. Ameumba mbingu ameumba nchi ameumba viumbe vyote,
  Bahari ni yake mito na milima ahimidiwe Mungu wetu
  Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo
  Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie