Anayekula Mwili Wangu

Anayekula Mwili Wangu
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
Composer(traditional)
Views36,920

Anayekula Mwili Wangu Lyrics

 1. Anayekula mwili wangu, na anywaye damu yangu
  Anaishi ndani yangu, 'ye hatakufa milele

  Yesu wangu nakuomba, nishibishe na mwilio
  Nayo damu yako ninywe, japo sistahili mimi

 2. Ndani yangu Mwokozi yumo kwa mwili na damu yake
  Ni rafiki yangu kweli nami sitamwacha kamwe
 3. Alikuja kutuokoa, tuliokuwa dhambini
  Kwa kifo chake msalabani, naye katupa uzima
 4. Yesu wangu unibariki, nifundishe njia zako
  Nipe moyo wa shukrani, nitembee nawe leo