Angalieni Sasa

Angalieni Sasa
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly

Angalieni Sasa Lyrics

Kwa maana angalieni sasa yametimia (yale yote)
Manabii walotabiri sasa yametokea (ona)

 1. Baba atamkana mama, mama atamkana Baba
  Watoto ni hivyo hivyo, tubuni tubuni sasa
 2. Magonjwa yasiyopona, uasherati wazidi
  Uzinzi na ubakaji, tubuni tubuni sasa
 3. Vita pande za dunia, bila sababu yoyote
  Watu waabudu fedha, tubuni tubuni sasa
 4. Njaa nayo itazidi ukame chakula hakuna
  Watu wateseka sana, tubuni tubuni sasa
 5. Neno litahubiriwa, pande zote za dunia
  Watu wamfuate nani, tubuni tubuni sasa
 6. Manabii wa uongo, watazunguka dunia
  Watawapotosha watu, tubuni tubuni sasa

  Tubuni tubuni sasa, tubuni tubuni sasa