Angalieni Sasa
| Angalieni Sasa | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Ikatetemeka Nchi (Vol 3) |
| Category | Tafakari |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 6,385 |
Angalieni Sasa Lyrics
Kwa maana angalieni sasa yametimia (yale yote)
Manabii walotabiri sasa yametokea (ona)- Baba atamkana mama, mama atamkana Baba
Watoto ni hivyo hivyo, tubuni tubuni sasa - Magonjwa yasiyopona, uasherati wazidi
Uzinzi na ubakaji, tubuni tubuni sasa - Vita pande za dunia, bila sababu yoyote
Watu waabudu fedha, tubuni tubuni sasa - Njaa nayo itazidi ukame chakula hakuna
Watu wateseka sana, tubuni tubuni sasa - Neno litahubiriwa, pande zote za dunia
Watu wamfuate nani, tubuni tubuni sasa - Manabii wa uongo, watazunguka dunia
Watawapotosha watu, tubuni tubuni sasa
Tubuni tubuni sasa, tubuni tubuni sasa