Asante Bwana kwa ukarimu
   
    
     
         
          
            Asante Bwana kwa ukarimu Lyrics
 
             
            
- Asante Bwana kwa ukarimu wako wa ajabu,
 Na fadhili zako hazina mipaka,
 Sina budi kusema Bwana asante
 Umenijua Bwana kabla sijazaliwa
 Maisha yangu umeweka kwenye msitari
 Kwa maana umenipenda, umenijali
 Nakushukuru ee Bwana asante *2
- Ninapotafakari upendo wako kwangu mimi
 Na riziki zangu wanipa kila siku
 Nashindwa nikulipe nini ee Bwana
- Na mwili wangu umenipa akili ya kutosha
 Kuliko wanyama utashi umenipa
 Ufananishwe na nani ee Bwana
- Uhai wangu umenipa na sasa niko hai
 Wengi wamezikwa mimi bado nahema
 Nikulipe nini kwa upendo wako
- Na marafiki ndugu jamaa Bwana umenipa
 Dhiki zikinizidi wanifariji
 Upendo wako Bwana unanishangaza.
- Kwa hayo yote siwezi lipa langu shukrani
 na mengi bado hata siwezi kusema
 Bwana unayotenda kwangu makuu