Asante Mungu Baba

Asante Mungu Baba
Choir-
CategoryThanksgiving / Shukrani

Asante Mungu Baba Lyrics

Asante Mungu Baba, Mungu wangu asante
Kwa kunipa uzima, Baba asante sana
Umenilinda mimi, wanipa na riziki
Mimi nikushukuruje kwa mema yako *2

  1. Nikushukuru Baba nasema asante Mungu wangu
    Maana wewe wanilinda mchana hata usiku
  2. Akili yangu na ikutungie nyimbo nzuri sana
    Maana wewe ndiye unifanyiaye maajabu
  3. Umenilinda wiki nzima, nasema asante Bwana
    Umenikinga na hatari zote Bwana nashukuru