Asilegee Moyowe
Asilegee Moyowe | |
---|---|
Alt Title | Asiregee Moyowe |
Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | (traditional) |
Video | Watch on YouTube |
Views | 28,734 |
Asilegee Moyowe Lyrics
- Asilegee moyowe, asitokwe machozi,
Akimkumbuka Munguwe, kwa yake makombozi,
Mtoa roho msalabani, mtaka kufa mwenyewe,
Kwa sababu kumpenda ni, nani mfunga moyowe? - Bustani mle Getsemani, amwomba Mungu Baba,
Je mtu Mungu ana nini?, nguvu zake ni haba,
Rabbi wangu waziona, dhambi za binadamu,
Mwili wako umetona, kama jasho la damu. - "Salamu Rabi salamu", anena Yuda mbaya,
Mwenye moyo wake mgumu, ambusu pasi haya,
Aliwaambia “basi, ntakayembusu ndiye,
Mtwaeni na kwa upesi”, Yuda nani nisiye. - Yuda nani ila yeye, aliyetenda dhambi?
Akikosa kwa Munguwe, mtenda kwa hia na mbi,
Mwenye kumtendea mema, mtaka dhambi haoni,
Kwamba ni kutupa neema, kumwendea shetani. - Wote ni kupiga mbio, mitumewe pamoja,
Wamtia mikono yao, askari walokuja,
Wampeleka hukumuni, aamuliwe na mtu,
Ye kutoka uwinguni, Mwanzi mkuu wa watu. - Mtume Petri amkanusha, amenena “simjui”,
Uhodari umekwisha, machoye hainui,
Pilato amwona Rabbi, hakukosa 'ta neno,
Asema “sioni dhambi”, lakini ni mwoga mno. - Athubutu kumwachia, “si hukumu” aomba,
“Mmoja nitamfungulia, Yesu au Baraba,
Wayahudi mwamtakani?", “Baraba aachwe tu,
Yesu afe msalabani, damuye juu yetu” - Pilato “hukumu gani? simo nanawa mkono,
Mkimtaka Yesu mwueni”, la mwamzi hilo neno,
Mara askari wamwanza, ni kupiga kelele,
Kumcheka na kumchokoza, mwenye mema milele.
Asiregee Moyowe is a traditional piece.
The piece has been harmonized and arranged by various composers, the most common piece being John Mgandu's harmony (1986) based on a French traditional melody, “Jésus-Christ monte qu Calvaire”.
The song has been recorded by several choirs among them St. Patrick Morogoro, St. Augustine Mavurunza Dsm