Bahati Bahati

Bahati Bahati
Alt TitleBahati Imwagukie Nani
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJ. C. Shomaly

Bahati Bahati Lyrics

 1. Hii ndiyo siri ya maisha mema,
  Na tena utamu wa kumjua Yesu
  Bahati kaacha karamu kubwa

  { Bahati bahati nayo imwangukie nani
  Bahati bahati aliyeipata ni nani
  Imeandaliwa kwa wote wenye moyo safi
  Simama uonje na! moyo wako utasisimka } *2

 2. Wateule mbona mnasitasita,
  Hana ubaguzi wote awaita
  Bahati kaacha karamu kubwa
 3. Kama una dhambi nenda ukatubu,
  Bwana hakatai mtu atubupo
  Bahati kaacha karamu kubwa
 4. Kama u mgonjwa Bwana anaponya,
  Kama una njaa utapata shibe
  Bahati kaacha karamu kubwa
 5. Yote ya dunia yakikukabili,
  Piga moyo konde nenda kwake Bwana
  Bahati Kaacha karamu kubwa.