Baragumu la Maria

Baragumu la Maria
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumBaragumu la Maria
CategoryBikira Maria
ComposerBernard Mukasa
Views11,782

Baragumu la Maria Lyrics

  1. Nawakaribisha viumbe wa dunia tumuimbie -
    Nawakaribisha viumbe wa dunia tumuimbie
    Kwa kuwa wokovu wetu umepitia, tumboni mwake
    Ndiye simu ya neema toka kwa Baba, kuletwa kwetu

    Tumpigie ngoma, vinanda na baragumu
    {Mama Maria (salamu)
    Mama wa Yesu (Maria)} *4
    Pigeni kelele za shangwe, shangilia
  2. Mnaokubali kwamba Yesu ni Bwana na Mungu wenu
    Hebu fikirini ana thamani gani, mzazi wake
    Mama pekee aliyejaliwa mimba, kutoka juu

    Tumpigie ngoma vinanda na baragumu
    {Mama Maria (salamu)
    Mama wa Yesu (Maria)} *4
    Kwa ngoma na matarumbeta furahia
  3. Alimbadilisha nepi Bwana wetu Mwokozi wetu
    Akamuogesha tunayemuabudu, mwana wa Mungu
    Anajua kula yake na vaa yake, na lala yake

    Tumpigie ngoma vinanda na baragumu
    {Mama Maria (salamu)
    Mama wa Yesu (Maria)} *4
    Kwa kinanda cha nyuzi kumi, sherekea
  4. Ulimwengu ungeijua siri hii, na tungepona
    Sote tungekubali kusali rozari, tungeokoka
    Amani ingepatikana duniani, tungefurahi

    Tumpigie ngoma vinanda na baragumu
    {Mama Maria (salamu)
    Mama wa Yesu (Maria)} *4
    Kwa filimbi na kwa nzumari, changamka