Bwana Amejaa Huruma

Bwana Amejaa Huruma
Performed bySt. Cecilia Zimmerman
AlbumNimezitambua Hila (Vol 5)
CategoryZaburi
ComposerJ. C. Shomaly
Views7,030

Bwana Amejaa Huruma Lyrics

  1. Bwana amejaa huruma (amejaa)
    Bwana amejaa huruma na neema

  2. Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,
    Naam vyote vilivyomo ndani yangu
    Vilihimidi jina lake takatifu
  3. Akusamehe maovu yako
    Akuponye magonjwa yako yote
    Akutie taji ya fadhili na rehema
  4. Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,
    Na hukumu kwa wote wanaoonewa
    Alimjulisha Musa njia zake
  5. Bwana amejaa huruma na neema
    Haoni hasira upesi
    Ni mwingi wa fadhili na rehema