Bwana Anakuja
Bwana Anakuja |
---|
Performed by | - |
Category | Majilio (Advent) |
Composer | F. A. Nyundo |
Views | 15,956 |
Bwana Anakuja Lyrics
- Bwana anakuja, twendeni kumlaki,
Bwana Mungu wa Majeshi
Ziwasheni nyoyo, tumkampokee,
huyu mwenye utukufu
Karibu Bwana njoo, Karibu Bwana njoo
Shinda pamoja nasi
- Wewe ndiwe mkate, mkate wa mbinguni,
utulishe wenye njaa
Wewe ndiwe mwanga, sisi tu vipofu,
tufanye tuone tena
- Wewe ndiwe njia, tutakufuata,
turudi kwa Baba yetu,
Wewe ni ukweli, utuangazie,
tusije tukapotoka
- Wewe ni uzima, sisi tu wagonjwa,
twakujia utuponye
Tumwendee nani, tukielemewa,
kitulizo chetu wewe
- Wewe ni mzabibu, sisi tu matawi,
tuungane siku zote
We mchungaji mwema, tunakutambua,
tuongoze malishoni
- Bado tu njiani, yadumu imani,
tumaini na upendo
Saa ya kufa kwetu, tupate kuona,
uso wako wa rehema