Bwana Anakuja

Bwana Anakuja
Choir-
CategoryMajilio (Advent)
ComposerF. A. Nyundo

Bwana Anakuja Lyrics

 1. Bwana anakuja, twendeni kumlaki,
  Bwana Mungu wa Majeshi
  Ziwasheni nyoyo, tumkampokee,
  huyu mwenye utukufu

  Karibu Bwana njoo, Karibu Bwana njoo
  Shinda pamoja nasi

 2. Wewe ndiwe mkate, mkate wa mbinguni,
  utulishe wenye njaa
  Wewe ndiwe mwanga, sisi tu vipofu,
  tufanye tuone tena
 3. Wewe ndiwe njia, tutakufuata,
  turudi kwa Baba yetu,
  Wewe ni ukweli, utuangazie,
  tusije tukapotoka
 4. Wewe ni uzima, sisi tu wagonjwa,
  twakujia utuponye
  Tumwendee nani, tukielemewa,
  kitulizo chetu wewe
 5. Wewe ni mzabibu, sisi tu matawi,
  tuungane siku zote
  We mchungaji mwema, tunakutambua,
  tuongoze malishoni
 6. Bado tu njiani, yadumu imani,
  tumaini na upendo
  Saa ya kufa kwetu, tupate kuona,
  uso wako wa rehema