Bwana Atuita

Bwana Atuita
ChoirOur Lady of Guadalupe
AlbumMisa - Guadalupe
CategoryEkaristia (Eucharist)

Bwana Atuita Lyrics

Bwana atuita - Bwana Yesu atuita
Tujongee mbele yake tukampokee

 1. Mwili wako ee Bwana damu yako ee
  Bwana yatushibisha roho zetu
 2. Karamu yako ni chakula cha kweli,
  Karamu yako ni kinywaji cha kweli
 3. Karamu yako ni kumbukumbu ya mateso
  Karamu yako ni karamu ya sadaka
 4. Karamu yako ni mwanakondoo wa kweli
  wa sadaka
  Karamu yako ni maana kweli katika safari yetu
 5. Karamu yako ni imani ya ufufuko wako
  Karamu yako ni mfano wa karamu ya mbinguni
 6. Karamu yako ni dawa ya udhaifu wetu
  Karamu yako ni malisho ya mchungaji