Bwana Nakupenda Lyrics

BWANA NAKUPENDA

Bwana nakupenda we Mungu wangu
Pembe ya wokovu na nguvu yangu
Wewe ndiwe mwamba na jabali langu
Nakimbilia kwako Mwokozi wangu
Bwana ndiye kinga na ngao yangu
Yeye ndiye mwamba na ngome yangu
Bwana ndiye kinga na ngao yangu
Sitaogopa nimwogope nani
{Kwa hiyo nitamwita astahili sifa
aniokoe na adui zangu *2

 1. [t/b] Asifiwe Mungu aliye hai atukuzwe Mungu wokovu wangu
  [s/a] Asifiwe mwamba wa usalama, atukuzwe kati ya mataifa
  [t/b] Ampa mfalme wokovu wote, wokovu mkuu ampatia
  [s/a] Amfanyia fadhili masihi humjalia mteule wake
  [t/a] Kwa hiyo nitaliimbia sifa jina lako Mungu wangu
 2. Kamba za kifo zilinizingira, maangamizi yalinivamia
  Kamba za kuzimu zilinisonga, mitego ya kifo ilinikabili
  Katika tabu nilimwita Mungu nilimlilia anisaidie
  Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake alisikia
  Kilio changu kilimfikia masikioni mwake
 3. Hapo ndipo dunia ikatetemeka ilihangaika na kutikisika
  Misingi ya milima ikayumbayumba Mungu alikuwa amekasirika
  Moshi ulishuka puani mwake moto uvunjao kinywani mwake
  Aliinamisha anga akashuka chini na wingu jeusi miguuni pake
  Makaa mengi ya moto yakalipuka kutoka kwake
 4. Mungu alinguruma kutoka mbinguni mkuu akatoa sauti yake
  Alipulika giza mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka
  Huko mawinguni makaa ya moto mvua ya mawe zikatokea
  Alirusha umeme ukawapiga maadui zake wakatawanyika
  Hapo ndipo bahari na dunia zilipoonekana
 5. Mungu alinyoosha mkono wake kutoka juu akanichukua
  Katika maji mengi alininyanyua akanitoa kwa adui zangu
  Tegemeo langu ni Bwana Mungu aliniokoa na adui zangu
  Walioniwinda aliwatisha aliwakemea wakapotea
  Amenitoa hapo akanipeleka palipo na nafasi
Bwana Nakupenda
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMNakaza Mwendo (Vol 19-20)
CATEGORYZaburi
REFPs. 18
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments