Bwana Ni Ngome

Bwana Ni Ngome
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumNikiziangalia Mbingu (vol 18)
CategoryZaburi
ComposerD. J. Mallya
Views9,525

Bwana Ni Ngome Lyrics

  1. { Bwana ni ngome yangu na nguvu yangu
    Bwana ni nuru yangu nimwogope nani? } *2

  2. Watesi wangu na pia adui zangu
    Waliponikaribia wakaanguka
  3. Hata kama nikizungukwa na majeshi
    Sitaogopa vita sitakufa moyo
  4. Jambo moja ningemwomba Mwenyezi Mungu
    Nikae nyumbani mwake siku zote
  5. Niuone uzuri wa Mwenyezi Mungu
    Nikatafakari hekaluni mwako
  6. Nami nitawashinda maadui zangu
    Nitamshangilia hekaluni mwake