Ee Bwana Uisikie Haki Lyrics

EE BWANA UISIKIE HAKI

@ J. C. Shomaly

Ee Bwana uisikie haki, usikie haki
Utege sikio lako Bwana, kwa maombi yangu (Bwana)
{ Usikilize maombi yangu yasiyotoka katika,
Yasiyotoka katika midomo ya hila } *2

  1. Nyayo zangu zimeshikamana, zimeshikamana na njia zako,
    Hatua zangu haziku, hazikuondoshwa.
  2. Ee Mungu nimekuita wewe, kwa maana wewe utaitika,
    Utege sikio lako nisikie mimi.
  3. Unifiche chini ya uvuli, chini ya uvuli wa mbawa zako
    Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Ee Bwana Uisikie Haki
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMTazameni Miujiza (Vol 2)
CATEGORYZaburi
REFPs. 17
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE2
4
  • Comments