Ee Bwana Uisikie Haki

Ee Bwana Uisikie Haki
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumTazameni Miujiza (Vol 2)
CategoryZaburi
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,189

Ee Bwana Uisikie Haki Lyrics

  1. Ee Bwana uisikie haki, usikie haki
    Utege sikio lako Bwana, kwa maombi yangu (Bwana)
    { Usikilize maombi yangu yasiyotoka katika,
    Yasiyotoka katika midomo ya hila } *2

  2. Nyayo zangu zimeshikamana, zimeshikamana na njia zako,
    Hatua zangu haziku, hazikuondoshwa.
  3. Ee Mungu nimekuita wewe, kwa maana wewe utaitika,
    Utege sikio lako nisikie mimi.
  4. Unifiche chini ya uvuli, chini ya uvuli wa mbawa zako
    Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.