Bwana Unaweza

Bwana Unaweza
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumNakaza Mwendo (Vol 19-20)
CategoryTafakari
Views10,035

Bwana Unaweza Lyrics

  1. Vipofu, viziwi, na wakoma wakapona
    Makahaba wakaepuka kifo cha mawe
    Wenye harusi wakajaliwa divai
    Lazaro akafufuka siku ya tatu*
    Nimekuita kwa hofu siku nyingi sana
    Nimekulilia ili nisaidike
    Unaweza unaweza Bwana,
    Unaweza unaweza sana
    Nitazame nitazame upya,
    Nitazame kwa huruma yako

  2. Dhambi zangu zimegeuka mzigo kwangu
    Zinanizuia kuona hurumayo
    Unaweza unaweza Bwana
  3. Lakini niende wapi zaidi ya kwako
    Tena wewe una huruma ya milele
    Unaweza unaweza Bwana
  4. Nimekulilia siku nyingi nimeomba
    Shida zangu zinazidi kunilemea
    Unaweza unaweza Bwana
* tatu - New versions sing: Lazaro akafufuka siku ya nne