Bwana Unayoyatenda

Bwana Unayoyatenda
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJ. C. Shomaly
Views5,249

Bwana Unayoyatenda Lyrics

  1. { Bwana unayoyatenda kwangu mimi ni huruma ya kweli
    (ya kweli) sitakuwa na fadhila nisipokiri haya } *2
    { Kuniumba, bila ya kukwambia, akili yangu tofauti sana
    Ninalala pia ninaamka tazama niko hai } *2

  2. Uhai nilio nao, sijanunua lolote,
    Bwana nashukuru sana ninasema asante
  3. Marafiki umenipa, maisha ya kupendeza,
    Bwana nashukuru sana ninasema asante
  4. Umenipa na watoto, yote sikutarajia,
    Bwana nashukuru sana ninasema asante
  5. Yote umetenda kwangu, bila mimi kuwa mwema
    Bwana nashukuru sana ninasema asante