Bwana Yesu Alitamka
Bwana Yesu Alitamka Lyrics
- Bwana Yesu alitamka, mimi ndimi njia ya kweli
Mtu haji kwa Baba yangu, Ila kwa njia yangu mimi
Hebu jiulize (jiulize) njia gani uifuatayo
Nawe waelekea wapi na wafuata njia ya kweli
- Njia nyembamba yenye tabu, ndiyo iendayo Mbinguni
Na ile pana ya anasa, yaelekea Jehanam
- Ngamia ni rahisi sana, kuingia tundu la sindano,
Kuliko mtu mwenye dhambi kuingia Mbinguni kwa Baba
- Mimi ndimi mwanzo na mwisho, mimi Alfa na Omega
Mtu haji kwa Baba yangu, Ila kwa njia yangu mimi