Bwana Yesu Kazaliwa

Bwana Yesu Kazaliwa
Performed by-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
Composer(traditional)
Views15,600

Bwana Yesu Kazaliwa Lyrics

  1. Bwana Yesu kazaliwa, Tumwimbie kwa furaha, aleluya

    Aleluya aleluya aleluya aleluya aleluya

  2. Kwa ajili yetu sisi, amezaliwa kitoto, aleluya
  3. Amezaliwa kitoto, nasi tumepewa mwana, aleluya
  4. Utawala na uwezo, vimo mabegani mwake, aleluya
  5. Jina lake ndilo Baba, wa milele tena mfalme, aleluya
  6. Enzi yake ya kifalme, haitakuwa na mwisho, aleluya
  7. Anakalia kitiye, chake Daudi babaye, aleluya
  8. Furaha binti Sayuni, umpokee Bwana wako, aleluya
  9. Dunia na ifurahi, nchi na ishangilie, aleluya