Bwana yu Mwema

Bwana yu Mwema
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumIkulu ya Mbinguni
CategoryTBA

Bwana yu Mwema Lyrics

 1. Njooni wenzangu, tuimbe pamoja
  Njooni tumwimbie Bwana, kwa kuwa Bwana yu mwema *2
  Amenitendea mambo mema mengi
  Mambo mengi ya ajabu kweli Bwana yu mwema *2

  Haya njooni, njooni tumwimbie Bwana
  Tuimbe kwa shangwe, kwa shangwe na nderemo nyingi
  Vigelegele, tumpigie vigelegele hoyee hoye
 2. Njooni tumshangilie, kwa shangwe na nderemo
  tumpigie makofi, na vigelegele vingi
  kwa furaha tuimbe, filimbi tuvipige
  Tujifunge na vibwebwe, tumshangilie Bwana
 3. Nilikata tamaa kwamba nimeshashibndwa
  Bwana akanipa moyo, nami nikafanikiwa
  Akanipa uwezo, wa kuyashinda yote
  Nikashinda kwa kishindo, kweli Bwana yu mwema
 4. Bwana hakuniacha, watesi wafurahi
  Akawapiga kikumbo, kwa nguvu wakaanguka
  Nikamililia, Bwana Mungu wangu,
  Baba Baba wasamehe, hawajui watendalo
 5. Nguvu zaanza kwisha, sauti yakauka
  Wenzangu endeleeni kumsifu Mungu Baba
  Siyo kwamba natoka, au nimeshachoka
  Bali ninavuta nguvu, nije kumwimbia Bwana