Chenga ya Mwili
Chenga ya Mwili | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Kidole Juu (Vol 23) |
Category | Ubatizo |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 9,559 |
Chenga ya Mwili Lyrics
Nimempiga shetani chenga ya mwili
Kuisalimisha roho yangu kuisalimisha roho
Nimempokea Yesu moyoni mwangu
Nipate uzima wa milele ili niishi milele- Tazama nimebatizwa kwa nafsi tatu
Baba mwana naye Roho Mtakatifu
Nimempokea Kristu moyoni mwangu
Kwa mwili na damu yake nimeshibishwa - Nimempokea Roho Mtakatifu
Amenijaza mapaji mapaji saba
Nimeikiri imani, imani yangu
Nimemkana shetani na mambo yake. - Nikikumbuka kiapo cha ubatizo
Najionea fahari ya ukristu wangu
Nikikumbuka ungamo la dhambi zangu
Ninaukiri upendo wa Yesu Kristu. - Nimeshamweka kando, shetani mwovu
Aliye mpotoshaji wa mambo mema
Alishaniweka kwenye, imaya yake
Alinidanganya sana na mambo yake