Chereko Bwana Amefufuka
| Chereko Bwana Amefufuka |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Pasaka (Easter) |
| Composer | M. B. Msike |
| Views | 12,154 |
Chereko Bwana Amefufuka Lyrics
{ Chereko chereko chereko chereko( chereko)
Chereko chereko Bwana amefufuka } *2
- Ni siku ya tatu malaika wa Bwana
Akamwaambia Maria, Bwana amefufuka
- Petro Yohane waenda kaburini
Wakakuta kaburi, kaburi liko wazi
- Malaika kasema, nendeni Galilaya
Huko ndiko aliko, amewatangulia
- Ni siku ya furaha, ni siku ya amani
Chereko chereko Bwana amefufuka
- Nyimbo nzuri tuimbe, tukimsifu Mwokozi
Vigelegele na ngoma tuimbe aleluya