Dhambi Ilikuja
   
    
     
        | Dhambi Ilikuja | 
|---|
| Performed by | - | 
| Category | Tafakari | 
| Views | 5,131 | 
Dhambi Ilikuja Lyrics
 
             
            
- Mwokozi wetu Yesu twakuomba, sisi tu wanyonge
 Roho zetu twazitoa kwako, twakuomba utusaidie
 Twakuomba utuponyeshe.
- Dhambi ilikuja , dhambi ilikuja
 Dhambi ilikuja ulimwenguni ikatuletea magonjwa
 Dhambi imeondoa-usalama
 Dhambi imetuondolea nguvu
 Katuletea kifo na shida
 Dhambi imetutenga na Mungu
- Na mfano tutawapa, nyoka usipompasua kichwa
 Analetewa majani na mwenzake
 anapata joto na kwenda
- Twaenda kwa waganga twatoa kweli pesa nyingi sana
 Tunatibiwa na kuchanjachanjwa
 Twasahau mganga ni Yesu