Login | Register

Sauti za Kuimba

Ee Bwana Sistahili Lyrics

EE BWANA SISTAHILI

@ J. Sangu

EE BWANA SISTAHILI

{ Ee Bwana, sistahili
Sistahili ee Bwana uje moyoni mwangu } * 2
{ Lakini sema neno Bwana sema neno
(neno tu)
Nami nitajongea mbele kwa karamu } *2

 1. Karamu ya Bwana yatupa uzima
  Ni mwili wa Bwana na damu yake
 2. Hiki ni chakula kutoka Mbinguni
  Bwana atuita kutushibisha
 3. Huu mwili wangu hii damu yangu
  Njooni kwangu nami nitawalisha
 4. Siku zote Bwana atulisha sisi
  Kwa chakula bora kutoka Mbinguni
 5. Atukuzwe Baba atukuzwe Mwana
  Atukuzwe Roho Mtakatifu daima yote
Ee Bwana Sistahili
COMPOSERJ. Sangu
CHOIR
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
SOURCEMagomeni Tanzania
 • Comments