Tembea Nami Bwana
| Tembea Nami Bwana | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Kidole Juu (Vol 23) |
| Category | Tafakari |
| Composer | C. A. L. Ndomelo |
| Views | 10,215 |
Tembea Nami Bwana Lyrics
{Ee Bwana Mungu wangu
Tembea nami usiniache kwenye dunia (hiyo)
Ya machafuko } *2
Nikianguka, Bwana, uniinue Bwana
Nikiteleza, Bwana, unishike mkono
Uniepushe na maadui wa roho yangu
Uniepushe na maadui wa roho yangu- Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwa
(Kwani) Baadhi ya wanadamu wenzangu wamegeuka
Kuwa ni maadui zangu,
Wananiwinda wanikamate wavinyokoe viungo,
Eti wajipatie mali. - Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwa
(Kwani) Baadhi yawaathirika wenzangu wamekamatwa
Bwana na wameshauawa,
Wamewakata vichwa na mikono, na miguu yao Bwana,
Eti wajipatie mali - Tazama sisi wanao wakiwa twakimbilia (kwako)
(Kwako) twazikabidhi roho zetu mikononi mwako
Maana ni wewe kimbilio
Usituachie adui zako watutie mikononi
Bwana utushike mkono